TETESI za usajili barani Ulaya zinasema klabu ya Chelsea inataka kumsajili winga Rodrygo Silva de Goes maarufu Rodrygo na mshambuliaji Endrick Felipe Moreira de Sousa-Endrick waanaocheza Real Madrid na inajiandaa kuwasilisha maombi mawili yenye thamani pauni milioni 151.5 kukamilisha uhamisho. (Fichajes – Spain)

Dau kutoka Chelsea litakuwa na thamani ya pauni milioni 105.2 lakini Real Madrid haina nia ama kumuuza Rodrygo au Endrick. (Defensa Central – Spain)
Chelsea inatafakari kwa kina kulipa ada ya faini ili kujiondoa kwenye sharti la kumsajili Jadon Sancho moja kwa moja kutoka Manchester United, baada ya kutoridhishwa na kiwango cha winga huyo aliyekipiga kwa mkopo Stamford Bridge. (iNews)
Bournemouth ina matumaini kuzishinda Chelsea, Newcastle United na Tottenham Hotspur kupata Saini ya golikipa wa Liverpool, Caoimhin Kelleher. (The Sun)
0 Comments