Makonda aonya watakaopuuza msaada wa kisheria

 MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ameonya kuwa mwananchi yoyote atakayekaidi kupata suluhisho kupitia msaada wa kisheria wa Mama Samia atakamatwa na jeshi la polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa yule atakayetoa rushwa ili kupindisha maamuzi.

RC Makonda amesema hayo leo jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia ‘Samia Legal Aid Campaign’ itakayoendeshwa na timu ya wanasheria kwa siku kumi kwenye halmashauri saba za  mkoa huo.

Makonda amesema atashughulika na wakurugenzi watakaoshindwa kutatua changamoto zilizoibuka katika kampeni hiyo na kusisitiza heshima ya Samia legal Aid itunzwe.

“Hatutaki wanaposikilizwa wananchi halafu maagizo yakatolewa atokee kiongozi hataki kutatua mgogoro huo nitakula naye sahani moja,”amesema Makonda.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments