MOROCCO: Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Hemed Morocco amesema vijana wake walipambana vya kutosha lakini uzoefu uliisaidia Morocco kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Morocco na Taifa Stars zilichuana usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia 2026 kwenye Uwanja wa Honneir, Oudja, Morocco.
Taifa Stars inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa Kundi E, ikiwa na pointi sita katika michezo minne, Morocco ni kinara wa kundi hilo wakiwa na pointi 15.
0 Comments