Sheikh Walid awataka wananchi kuwekeza

SHEIKH Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Walid Alihad, amesema maendeleo ya jamii yoyote yanategemea uchumi na uwekezaji unaofanywa na nchi husika.

Akizungumza katika hafla hiyo ya Iftar jijini Dar es Salaam, ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo ya kuruhusu biashara kufanyika masaa 24 kwani itaongeza uchumi wa nchi yetu.

“Naipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuanzisha Zanzibar Sukuk, akihimiza wananchi kushiriki ili kuleta maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla. Hakuna kinachofanyika bila fedha—iwe misikitini, makanisani, viwandani au shuleni. Hii ni fursa ya maendeleo kwa wote,” amesema Sheikh Alihad.

Kwa upande wake, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Omary Kumbilamoto, alisema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan anataka kuhakikisha Dar es Salaam inakuwa na mwanga wa kutosha ili wafanyabiashara waweze kufanya kazi saa 24.

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa PBZ, Arafat Haji, amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi imeanzisha fursa hii kwa wananchi kuwekeza katika hatifungani inayozingatia misingi ya Sheria na Dini ya Kiislamu.

Arafat alieleza kuwa hatifungani hiyo inaleta faida ya asilimia 10.5 kwa mwaka kwa shilingi ya Tanzania, na asilimia 4.2 kwa mwaka kwa dola ya Kimarekani.

“Lengo la hatifungani hii ni kukusanya fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo Zanzibar, ikiwemo ujenzi wa maabara, viwanja vya ndege, bandari, na miradi mingine ya kimaendeleo,” amesema Arafat.

Ameongeza kuwa wananchi watakaowekeza watafaidika kwa kupokea faida kila baada ya miezi sita, na baada ya miaka saba, watarejeshewa mtaji wao wote pamoja na faida waliyoipata kwa kipindi hicho.

Pia, uwekezaji katika Zanzibar Sukuk unaweza kutumika kama dhamana kwa ajili ya mikopo katika taasisi nyingine za kifedha. SOMA: Tanzania yanga’ara uwekezaji kutoka nje

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments