KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuondoka alfajiri ya Ijumaa kuelekea Cairo, Misri kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhisi ya Al Masry ya nchini humo.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema wachezaji waliokuwa Morocco na Taifa Stars watajiunga moja kwa moja Misri tayari kwa mchezo huo wa kwanza wa robo fainali.
Kuhusu mchezo wa marudiano, Ally amesema: “Kaulimbiu ya mchezo dhidi la Al Masry itakuwa ni Hii Tunavuka. Hii inamaanisha kwamba kwa misimu mitano mfululizo tunaishia robo fainali lakini safari hii tunavuka kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu.
“”Viingilio vya mchezo dhidi ya Al Masry ni Mzunguko – 5,000, Orange – 10,000, Vip C – 15,000, Vip B – 30,000, Vip A – 40,000, Platinum – 150,000 na Tanzanite – 250,000. Tiketi zimeanza kuuzwa sasa.
“Niwatoe hofu kwamba Uwanja wa Benjamin Mkapa umeshafanyiwa ukaguzi. Bado majibu hayajatoka lakini katika mazungumzo wanasema kuna maboresho makubwa kwenye uwanja ukilinganisha na mara ya mwisho walipofanya ukaguzi hivyo kuna nafasi kubwa ya kucheza kwenye uwanja huo.”
0 Comments