Tanzania yajipanga na maamuzi ya Trump kuhusu ARV

Bohari ya Dawa (MSD), imesema kuwa Serikali imejipanga kukabiliana na changamoto zozote zitakazojitokeza kutokana na uamuzi wa Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump kusitisha misaada ya kwa nchi za Afrika.

Mapema mwaka huu, mara baada ya kuapishwa Rais Trump alitangaza kusitisha misaada yote iliyokuwa ikitolewa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) ikiwamo ugawaji bure wa dawa za kufubaza virusi vinavyosababusha ugonjwa wa Ukimwi (ARV).

Akizungumza kuhusu miaka minne ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumatano Machi 19, 2025, Mkurugenzi wa MSD, Mavere Tukai amessma kutokana na maelekezo ya Rais kwa MSD hakuna cha kusubiri.

"Tumeshafanya maandalizi ya kutosha kwa kuzingatia athari zake kwa wananchi.

“Tumehakikisha tunayo mikataba ya kutosha katika ununuzi wa dawa zote za miradi msonge ambayo inayokana na misaada ili ikitokea Marekani imesitisha Watanzania hawaathiriki na chochote,” alisisitiza Tukai.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments