Wananchi wa Longido waishukuru serikali kufunguliwa barabara ya Namanga-Mairouwa

Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeendelea kufungua fursa za kiuchumi kwa kuboresha miundombinu na kuondoa vikwazo kupitia mradi wa RISE sehemu ya uondoaji vikwazo katika barabara wilayani Longido mkoani Arusha.


Meneja wa TARURA wilaya ya Longido, Mhandisi Lawrence Msemo ameeleza kuwa mradi huo wa barabara ya Namanga - Sinonik - Mairouwa yenye urefu wa Km 9 na makalavati madogo 10 una mchango mkubwa kiuchumi kwa wakazi wa Mairouwa kwakuwa umerahisisha usafiri na usafirishaji wa mazao na bidhaa kwenda mpakani Namanga.

Naye, Diwani wa Kata ya Ngarneibo, Mhe. Simon Ngarioi ameipongeza serikali kwa kufanikisha uboreshaji wa barabara hiyo baada ya kuwa na hali mbaya kwa muda mrefu.

“Naipongeza serikali kwa kufanikisha ujenzi wa barabara hii na kuwawezesha wananchi wa Ngarneibo hasa kiuchumi na kurahisisha kusafirisha mizigo yao hadi Namanga, pia nahimiza wananchi kuitunza barabara hii ili idumu kwa muda mrefu", amesema.

Bw. Elia Laizer mkazi wa Ngarneibo ametoa shukrani zake kwa serikali kwa kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo kwa manufaa yao.

"Tunashukuru kwa barabara, hapo awali palikuwa ni pori, watu walikuwa wanashambuliwa na wanyama, magari yalikuwa yanakwama, lakini sasa muda wa kwenda Namanga kuuza na kununua bidhaa umepungua” .



TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments