Dalali: Hatutakubali Kombe liondoke

Zanzibar: Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali amesem hawatakubali Kombe la Shirikisho la Afrika liondoke.

Dalali ametoa kauli hiyo leo wakati wakifanya uhamasishaji wa mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho kati ya Simba na RS Berkane utakaochezwa Jumapili Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

“Mwaka 1993 mgeni alikuwa Mwinyi (Ali Hassan Mwinyi) kikombe kikaondoka, Jumapili mgeni tena Mwinyi (Dk Hussein ), halafu kikombe kiondoke hatukubali. Simba tunawakilisha nchi, mtu akitufanyia ubaya anahujumu nchi.

“Vijana hili kombe wanalitaka. Tuwape ushirikiano kwa kuwashangilia muda wote uwanjani. Tuna timu nzuri sana njooni tushangilie timu yetu. Tunamuomba Mwenyezi Mungu na sisi huu uwe mwaka wetu,” amesema Dalali.

Kwa upande wke Meneja wa Habari na Mawasiliano wa imba, Ahmed Ally, amesema wameshafanya maajabu mengi sana acha ya zamani.

“Msimu huu kila aliyetufunga na sisi tulimfunga. Berkane ameshamaliza zamu yake sasa ni zamu yetu. Hatuzungumzi haya sababu ya historia bali ubora ambao tupo nao.

“Tunakubali Benjamin Mkapa ndio ngome yetu lakini hatushindi sababu ya uwanja, tunashinda sababu ya ubora wetu. Uwanja wa Amaan ndio ulitupeleka fainali na sasa ndio utatupa ubingwa. Hatukumaliza deni na Hayati Rais Mwinyi (Ali Hassan) na sasa tunakwenda kulipa deni mbele ya mtoto wake, Rais Dk Hussein Mwinyi. Tunataka kulipa hili deni.”

“Tunafahamu kuna watu wanafanya kila hila Mnyama asichukue ubingwa lakini ifanye kwa kificho, tukikuona hatutakuacha salama. Hapa tulipo tumevua kabisa vazi la utu, tumevua vazi la ustaarabu. Hapa tulipo tumevaa unyama kwelikweli, tusitafutiane lawama. Hatutamuonea mtu aibu, tutakuharibia mazima.”

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments