Katika hotuba yake, Msita alisema, "Tusikimbiane kama tulivyofanya tarehe 8. Tukumbuke kuwa amani ni msingi wa maendeleo. Hakuna sababu ya kuruhusu hofu kutawala tena miongoni mwetu." Hata hivyo, hakufafanua moja kwa moja kilichotokea tarehe hiyo, lakini kauli yake ilionekana kuelekezwa kwa matukio ya kimechezo yaliyowahi kuvuruga utulivu katika baadhi ya maeneo.
Alisisitiza kuwa chama chake kipo tayari kusikiliza maoni ya wananchi na kushirikiana katika kuleta maendeleo ya kweli kwa kila Mtanzania. Aliwataka viongozi wa kisiasa kutumia majukwaa yao kuhubiri umoja badala ya uchochezi unaoweza kuchochea migawanyiko.
Wananchi waliokuwa wamehudhuria mkutano huo walionekana kuguswa na kauli hiyo, huku baadhi wakieleza kuwa ni muhimu kwa viongozi wote wa kisiasa kutoa kauli za kutuliza hali badala ya kuibua hisia kali miongoni mwa wananchi.
0 Comments