CCM BADO TUPO SANA ,TUNAYO AJENDA YA KUDUMU KUWATUMIKIA WATANZANIA-WASIRA

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Stephen Wasira ameeleza Chama hicho ni cha kudumu kwasababu kimekabidhiwa majukumu ya kudumu,hivyo kitaendelea kuwepo kwa ajilI ya kuwatumikia Watanzania.


Wasira ameyasema hayo leo Juni 16,2025 alipokuwa akizungumza na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita ambako ameanza ziara ya siku tatu ya kukagua uhai wa chama hicho na kuzungumza na wana CCM na makundi mbalimbali.

" CCM ni Chama kikubwa na chenye historia, watu wengi wanadhani CCM ilianza miaka 48 iliyopita ,Chama hiki kimerithi mikoba ya TANU na Afro Shiraz Party.TANU kina miaka 75 na Afro Shirazi Party miaka 67.

"CCM imekabidhiwa majukumu ya kudumu ya kuwatimikia Watanzania, hivyo ukisema kidumu Chama Cha Mapinduzi hatuna utani ,kwasababu kina majukumu ya kudumu ambayo tumekabidhiwa tangu kuanzishwa kwake,"ameeleza.

Ameongeza chama hicho kinadumu kwasababu kinakwenda na wakati , kinarithiwa vizazi na vizazi na ndio maana waliopo leo kwenye Chama wengi wao wakati kinaanzishwa hawakuwepo lakini kwa kuwa kinarithisha ndio maana wapo na wao watarithisha kwa wengine.

"Hakiwezi kudumu kama hakipokelewi na vizazi, hakiwezi kudumu kama hakina kazi za kudumu.Chama hiki kimetokana na TANU na Afro Shiraz Party vyama ambavyo vilikuwa na historia kubwa.Historia ya TANU ilisema ni kuwaandaa Watanzania kujitawala lakini kuondoa ubaguzi wa makabila, rangi na dini na kujenga umoja.

"Hivyo umoja ni kazi ya CCM tuliyokabidhiwa na sasa umoja na amani ya nchi yetu imekuwa tunu ya Watanzania wote .Kwahiyo ukianzisha jambo lako lilakolea na likakubaliwa na watu wote linakuwa lako lakini pia linakuwa la wote."

Wasira amesisitiza kazi ya chama hicho ni kuendelea kujenga umoja wa watu wote na kufafanua nchi ya Tanzania iko tofauti na mataifa mengine ya Afrika kwani nchini kwetu hakuna ukabila wala udini.

Katika hatua nyingine Wasira amewapongeza viongozi wa dini nchini kuhubiri amani kuelekea Uchaguzi mkuu mwaka huku akitoa rai kwa vipngozi hao kutohubiri siasa wanapokuwa nyumba za ibada kwa lengo la kuepuka malumbano.

Pia amesema kwa kuwa nchi yetu imefanikiwa kujenga misingi imara ya umoja imesababisha nchi watu wake kutobaguana kwa kabila,dini wala rangi.

“Viongozi wa dini Sheikh na Mchungaji wanakaa nyumba moja na wala hawagombani kwababu hatuna mambo ya udini.Viongozi wetu wa dini ukiona wanagombana basi itakuwa kwasababu ya Shetani sio Mungu.

"Koraani inamlaani Shetani na Biblia nayo inamlaani Shetani. Mungu anapenda mambo mema na Shetani anapenda mambo mabaya, ndio maana msikitini wanapambana na shetani na kanisani wanapambana na shetani.Nchi yetu haina dini lakini raia wake wa dini, wako Waislam ,wako Wakristo na wasio na dini wenyewe wanaabudu mizimu na wote wanalindwa.

"Ninachotaka kueleza hapa CCM imekabidhiwa kazi ya kulinda umoja na amani ya nchi, kwahiyo ninyi viongozi watu nataka muwaambie wale wanaotaka kuvunja umoja wa Watanzania waambieni wamepiga Wrong namba.”









TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments