Kada wa CCM Amsifia Rais Samia kwa Uongozi wa Kizalendo

                 
                                    
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Japhari Saidi, amempongeza kwa dhati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake wa kizalendo, wenye maono na maslahi mapana kwa wananchi kwa kipindi cha miaka minne.
Amesema Dkt. Samia ameendelea kutekeleza kwa mafanikio makubwa miradi mikubwa ya maendeleo iliyoanzishwa na watangulizi wake, huku akianzisha miradi mipya yenye tija katika sekta mbalimbali kama miundombinu, afya, elimu, maji, utalii, diplomasia na michezo. "Rais Samia ameonesha ujasiri, busara na dhamira ya kweli ya kuwatumikia Watanzania. Ameinua hadhi ya nchi yetu kimataifa na pia ameweka nguvu kubwa katika michezo, jambo linalowapa vijana motisha na fursa mpya," alisema Kada Japhari. Aidha, alitoa wito kwa Watanzania kuendelea kumuunga mkono Rais Samia ili kuendeleza kasi ya maendeleo na kudumisha amani nchini.
                                      
                                     
Na Abdul Ramadhani Singida

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments