Lwanji amebainisha kuwa zoezi hilo litadumu kwa siku tano tu, na amesisitiza kuwa hakuna haja ya bwembwe au kampeni za aina yoyote wakati wa kuchukua fomu, kwani hatua hiyo si kampeni bali ni sehemu ya mchakato wa kawaida wa kidemokrasia ndani ya chama.
"Zoezi la kuchukua fomu ni la kawaida, siyo kampeni. Wanachama wote wenye sifa wanayo haki ya kuchukua na kuchaguliwa bila bughudha yoyote," amesema Lwanji.
Kwa upande mwingine, vijana wa CCM mkoani Singida wametajwa kuwa wameandaliwa vizuri na kufundwa vya kutosha kwa ajili ya kushiriki kikamilifu katika usimamizi na uhamasishaji wa uchaguzi huo, wakilenga kudumisha nidhamu, amani na mshikamano ndani ya chama.
Mwenezi huyo pia amesisitiza kuwa mchakato mzima wa uchaguzi utafanyika kwa haki, na uteuzi wa wagombea utafanyika kwa kuzingatia taratibu rasmi za chama, kwa lengo la kupata viongozi bora, wenye uwezo wa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM na kutetea maslahi ya wananchi.
Na Mwandishi wetu Singida
0 Comments