Kundi la zaidi ya majaji 100 kutoka Mahakama ya Rufani nchini limetembelea Kijiji cha Nyuki kilichopo Kisaki, Singida na kufurahishwa na mazingira ya kipekee ya eneo hilo ambalo limebeba utalii wa asili na elimu ya uhifadhi wa nyuki.
Katika ziara hiyo, majaji hao walipata fursa ya kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa katika kijiji hicho ikiwa ni pamoja na kuonja vyakula vya asili, kutembelea mashamba ya mazao mseto yanayolimwa kwa kutumia mbinu rafiki kwa mazingira na kushuhudia uhusiano wa kirafiki baina ya nyuki na binadamu.
Mkurugenzi na mwanzilishi wa Kijiji cha Nyuki, Bw. Philimoni Kiemi, aliwaongoza wageni hao na kutoa semina fupi kuhusu umuhimu wa nyuki katika mfumo wa ikolojia, uhifadhi wa mazingira, na fursa za kiuchumi zinazotokana na ufugaji wa nyuki.
“Nyuki ni viumbe muhimu kwa maisha ya binadamu na mazingira yetu. Kijiji hiki kimejengwa kwa dhima ya kutunza mazingira na kutoa elimu kupitia utalii wa kiikolojia,” alisema Bw. Kiemi.
Majaji hao walionyesha kufurahishwa na ziara hiyo huku wakieleza kuwa kijiji hicho ni mfano wa kuigwa katika kuendeleza utalii wa ndani unaolenga uhifadhi na maendeleo ya jamii.
Majaji Zaidi ya 100 Wavutiwa na Kijiji cha Nyuki Kisaki – Singida
Karibu Kijiji cha Nyuki Kisaki – Kituo cha Utalii wa Asili Kanda ya Kati!
Majaji wa Mahakama ya Rufani Wavutiwa na Huduma, Mazingira na Elimu ya Nyuki!
Philimoni Kiemi: "Nyuki Ni Rafiki wa Binadamu – Na Chanzo cha Uchumi Endelevu
Mazao ya Asili, Chakula Kitamu, Elimu ya Mazingira – Vyote Kipo Kisaki Singida
Kisaki ni Zaidi ya Kijiji – Ni Shule, Ni Mapumziko, Ni Urithi Wetu
Abdul Ramadhani Singida
TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI
Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516
0 Comments