Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi jimboni humo, Chief Mgonto alibainisha kuwa dhamira ya CCM ni kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia maslahi ya jamii na taifa kwa ujumla.
Amesema kipaumbele chake ni kuhakikisha kila sekta muhimu—elimu, afya, barabara, kilimo na maji—inaendelea kupiga hatua ili kuongeza ustawi wa wananchi wa Ikungi Mashariki.
Aidha, Mgonto amewataka wananchi kuendelea kuiamini CCM kwani ndiyo chama pekee chenye historia, uzoefu na uthubutu wa kuwaletea maendeleo ya kweli.
Pia aliwahimiza kumpigia kura mgombea urais kupitia CCM, wabunge na madiwani, akisema viongozi bora na wenye kuenzi amani ya taifa wanatokana na CCM.
Wananchi walipokea kwa hamasa kubwa ujumbe wa Mgonto, wakiahidi kumpa ushirikiano ili kuendeleza kazi kubwa ya maendeleo iliyofanywa na serikali ya awamu ya sita.
Matukio kwa Picha
Alifu Abdul Singida Ikungu
0 Comments