KATIBU MKUU UWT AWAHIMIZA WANACHAMA KILOLO KUJITOKEZA KUPIGA KURA ZOTE KWA CCM

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Taifa Ndg. Suzan Peter Kunambi (MNEC), amewahimiza wanachama kujitokeza kwa wingi kupiga kura nyingi za  ndio hata kama kuna sehemu kuna mgombea amepita bila kupingwa.

Katibu Kunambi ameyabainisha hayo wakati wa   mkutano wa ndani katika Kata ya Nyalumbu, Wilaya ya Kilolo,Mkoa wa Iringa ambapo amesema wanachama wanapaswa kutofanya makosa na badala yake kumpa kura nyingi za kishindo Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

"Kitu kikubwa ambacho ninawaomba wanachama wa ccm wa kilolo hususan wanawake tunapaswa kuwa mstari wa mbele katika kupiga kura za ndio hata kama mgombea fulani amepitwa bila kupimgwa,"amebainisha Katibu huyo.

Amebainisha kwamba ni vema kuweka mikakati kabambe ambayo itaweza kukisaidia chama cha mapinduzi kiweze kupata ushindi wa kishindo katika Mafiga matatu ambayo ni nafasi ya Urais,Udiwani pamoja na Ubunge.

Aidha amesisitiza kuwepo kwa mshikamano wa pamoja kati ya  wanachama wa CCM pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika octoba 29 mwaka huu.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments