KINGU NI HAZINA KWA IKUNGI NA TAIFA,ASEMA MWIGULU

                                     

Katika uzinduzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Ikungi Magharibi, Waziri wa Fedha  Dkt. Mwigulu Nchemba, amesisitiza umuhimu wa wananchi kuendelea kuunga mkono wagombea wa CCM kwa nafasi zote.

Akizungumza akiwa ameambatana na mgeni rasmi wa uzinduzi huo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, Dkt. Mwigulu alimuelezea Mbunge Kingu kama mbunge makini, mwenye hoja zenye mashiko, mchango wa hali ya juu bungeni, na mwenye kuchangamka katika kila mjadala. Alisisitiza kuwa Kingu ni kiongozi asiyechoka kupigania masilahi ya wananchi wake na Taifa kwa ujumla.  

                                        

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson naye aliongeza kuwa Kingu ni hazina kubwa kwa wananchi wa Ikungi na Tanzania nzima, akihimiza wananchi wa jimbo hilo kumpa kura za kishindo ili aendelee kuwatumikia kwa uadilifu na ufanisi mkubwa.

Aidha, viongozi hao waliwaasa wananchi kutambua mchango mkubwa wa CCM katika kuleta maendeleo ya nchi kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza miradi ya kimkakati ikiwemo elimu, afya, maji, barabara na nishati.

                                           

Kwa pamoja walisisitiza kuwa CCM ina wagombea makini kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge hadi Udiwani, wagombea wanaojali masilahi ya wananchi na kuhakikisha kila eneo linashiriki kikamilifu katika ajenda ya maendeleo ya taifa.

                                            

Wananchi wa Ikungi na Tanzania kwa ujumla wakahimizwa kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi huu, na kwa kifua mbele kumpigia kura mgombea wa Urais kupitia CCM, wagombea wa Ubunge akiwemo Kingu, pamoja na madiwani wote wa CCM ili kuhakikisha chama kinapata ushindi wa kishindo na kuendelea kusimamia amani, mshikamano na maendeleo endelevu ya Watanzania.

Na alifu Abdul Singida Ikungi

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments