Nyota wa soka wa TRA United, Ramadhani Salum maarufu kama Chobwedo, ameendelea kuwa gumzo nchini baada ya kupokea zawadi maalum kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Amos Gabriel Makalla, aliyemtaja wazi kuwa ni mali muhimu ya soka la Tanzania kutokana na kiwango chake bora msimu huu.
Katika tukio hilo lililofanyika Arusha Jumanne Aprili 21, 2026, RC Makalla alikutana na nyota huyo wa TRA United, akazungumza naye kwa karibu na baadaye kumpatia zawadi ya viatu vya kisasa aina ya Nike pamoja na vitu vingine mbalimbali kama sehemu ya kumtia moyo kuendelea kung’ara.
Makalla ambaye pia ni mlezi wa TRA United, alisema amefurahishwa mno na kiwango ambacho Chobwedo amekuwa akikionesha katika mechi kubwa za Ligi Kuu Tanzania Bara, hasa dhidi ya Young Africans S.C., Simba SC na Pamba Jiji FC. na Singida Black Stars
Alisema kuwa mchezaji huyo ana kipaji kikubwa, nidhamu ya kazi na uwezo wa kubadili mchezo muda wowote, jambo linalomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wa kutegemewa zaidi kwa sasa.
Nikisema huyu ni mali, basi ni mali kweli. Nimecheza mpira, nimefundisha mpira, najua ninachokisema. Chobwedo ni mchezaji mkubwa,” alisema Makalla.
Pia alimshauri kijana huyo kutokata tamaa kutokana na maneno ya mitandaoni, akimtaka kubaki makini, kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kujijenga zaidi kisoka.
KUTOKA MITAA YA SINGIDA HADI JUKWAA LA TAIFA
Wengi wanaomwona leo akifanya makubwa huenda hawajui safari halisi ya Ramadhani Chobwedo. Nyota huyo ni mzaliwa wa Singida, alikulia katika maeneo ya Kibaoni na Majengo ndani ya Manispaa ya Singida.
Katika utoto wake, Chobwedo alikuwa sehemu ya vijana waliopenda soka kila siku mitaani na viwanjani. Aliwahi kuonekana akicheza katika viwanja mbalimbali vya kihistoria vya Singida ikiwemo:
Uwanja wa Kibaoni
Uwanja wa Ipembe Secondary School
Uwanja wa Ukombozi Primary School
Uwanja wa Mwenge Secondary School
Bombadia (zamani People’s)
Liti (zamani Namfua)
Na Uwanja Wa Shule ya Msingi Sumaye ilioko jirani na kituo cha Polisi Singida.
Chobwedo :Timu za Mtaa alipitia kwa kocha Aalimaarufu (MTIPA) na (STONE IGWE) wote wanajishughulisha na timu za vijana mkoani Singida.
Ni katika viwanja hivyo ndipo ndoto yake ilianza kuonekana mapema, huku wengi wakimuona kama kijana mwenye kasi, mbinu na uwezo wa kuwazidi mabeki kirahisi.
KUHAMIA ARUSHA NA KUFUNGUKIWA MILANGO
Baadaye Chobwedo alihamia Arusha ambako aliendelea kupambana kutafuta nafasi katika soka la ushindani. Huko ndiko safari yake ilipoanza kubadilika rasmi.
Kupitia juhudi, nidhamu na kujituma, alianza kujijenga hadi kufikia kuchezea TRA United, timu ambayo sasa imekuwa nyumbani kwake kisoka.
Ndani ya msimu huu, Chobwedo ameonyesha kiwango cha juu sana kiasi cha kuwa mchezaji anayezungumziwa zaidi kwenye ligi.
TUZO ZA MAN OF THE MATCH ZAMPA UMAARUFU
Msimu huu tayari Ramadhani Chobwedo ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mechi (Man of the Match) mara kadhaa, akifanya hivyo dhidi ya:
Tanzania Prisons SC
Young Africans S.C.
Singida Black Stars
Uwezo wake wa kupiga chenga, kasi pembeni, kupenyeza mipira na kutengeneza nafasi za mabao umeifanya timu nyingi kuanza kumfuatilia kwa karibu.
VIGOGO WAANZA KUMUWANIA
Kutokana na kiwango chake, taarifa mbalimbali zinaeleza kuwa baadhi ya vigogo wa soka Tanzania wameanza kuonyesha nia ya kumtaka kwa msimu ujao.
Mashabiki wengi wanaamini kama ataendelea na kiwango hiki, Chobwedo anaweza kuwa mmoja wa mastaa wakubwa wa soka la Tanzania ndani ya muda mfupi.
BANDOLAMEDIA TUNAKULETEA ZAIDI
Safari ya Ramadhani Chobwedo haijaanza leo. Ni simulizi ya kijana aliyepitia changamoto, akaamini kipaji chake na sasa anavuna matunda mbele ya taifa.
Kupitia makala maalum za BandolaMedia, tutakuletea mahojiano ya kipekee ya Chobwedo akizungumzia:
Alikotoka
Changamoto alizopitia
Siri ya mafanikio yake
Ndoto zake za baadaye
Timu anayoitamani kuchezea
Endelea kufuatilia BandolaMedia kwa habari, makala na exclusive stories za michezo.
Abdul Ramadhani Tanzania

0 Comments