CHIEF THOMAS MGONTO AKUTANA NA WAZEE MISUGHA, AZUNGUMZA KINYATURU AKINYWA NAO KAHAWA | SIKONGA NA CHIEF

                                  

Mbunge wa Jimbo la Ikungi Mashariki, Chief Thomas Mgonto, ameendelea na ziara yake ya "Sikonga na Chief na Tukutane Kitaa", ambapo leo alikutana na wazee wa eneo la Misugha kwa mazungumzo ya karibu yaliyofanyika katika mazingira ya kawaida huku wakinywa kahawa pamoja.

Katika kikao hicho, Chief Mgonto alizungumza na wazee hao kwa lugha ya Kinyaturu, hatua iliyowafanya wajisikie karibu zaidi na kiongozi wao na kutoa fursa ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Jimbo la Ikungi Mashariki.

Akizungumza na wazee hao, Mbunge Mgonto aliwakumbusha kuwa dhamana waliompa ya kuwawakilisha Bungeni ndiyo msingi wa kazi anayoendelea kuifanya kila siku. Alieleza kuwa sauti za wananchi wa Ikungi Mashariki zimeendelea kufikishwa katika vikao vya maamuzi kupitia hoja, ushauri na michango yake bungeni kwa lengo la kutetea maslahi ya wananchi na kuharakisha maendeleo ya jimbo.

Aidha, aliwahimiza wananchi kuendelea kushirikiana, kudumisha umoja na kutoa maoni yao kwa uwazi ili yaweze kusaidia kupanga na kutekeleza vipaumbele vya maendeleo vinavyoendana na mahitaji halisi ya jamii.

Kwa upande wao, wazee wa Misugha walieleza kufurahishwa na utaratibu wa Mbunge wao kufika moja kwa moja miongoni mwa wananchi badala ya kusubiri mikutano mikubwa pekee. Walisema mazungumzo ya ana kwa ana yanajenga uaminifu, yanaimarisha ushirikiano na yanatoa nafasi kwa wananchi kueleza changamoto na mapendekezo yao kwa uwazi.

Ziara ya "Sikonga na Chief na Tukutane Kitaa" inaendelea katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Ikungi Mashariki ikiwa na lengo la kuimarisha mawasiliano kati ya mbunge na wananchi, kusikiliza maoni yao na kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya uwakilishi kwa maendeleo ya jimbo.

Picha Mbali Mbali katika matukio ya "Sikonga na Chief na Tukutane Kitaa"

                                        








Na Abdul Ramadhani Tanzania

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments