MAKAMU WA RAIS KUFUNGUA MKUTANO WA 46 WA CATA JIJINI ARUSHA

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius John Ndejembi, amewasili mkoani Arusha leo, Jumatatu, Oktoba 5, 2026, kwa ajili ya kufungua Mkutano wa 46 wa Chama cha Wasimamizi wa Kodi wa Jumuiya ya Madola (CATA).

Makamu wa Rais amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), ambako amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla, pamoja na viongozi wengine wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali.

Mkutano huo utafanyika katika Ukumbi wa Grand Melia jijini Arusha na unatarajiwa kuwakutanisha viongozi na wataalamu zaidi ya 400 kutoka mataifa 48.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments