Wizara ya Madini na taasisi zake imeendelea kuhamasisha watumishi kufanya mazoezi ya mwili kupitia bonanza la michezo linalofanyika mara kwa mara, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha afya zao, kujenga umoja na kuongeza ufanisi katika utendaji wa kazi.
Akizungumza leo jijini Dodoma wakati wa bonanza hilo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo, amesema sekta ya madini ni miongoni mwa sekta muhimu katika kukuza uchumi wa taifa, kuongeza fursa za ajira na kuboresha maisha ya Watanzania.
Mbibo amesisitiza kuwa mazoezi ya mwili yanapaswa kuwa sehemu ya maisha ya kila siku, akiwataka watumishi wa wizara hiyo na taasisi zake kuweka kipaumbele katika kutunza afya zao kwa kufanya mazoezi mara kwa mara.
Amesema kuwa afya njema ni msingi muhimu wa utendaji wenye tija, hivyo ni wajibu wa kila mtumishi kuhakikisha anajenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kujikinga na magonjwa mbalimbali yasiyoambukiza.
“Tukifanya mazoezi tutahakikisha kwamba tunaepukana na magonjwa mbalimbali yasiyo ya kuambukiza,” amesema Mbibo.
Aidha, ametoa wito kwa watumishi kuendelea kushiriki katika shughuli za michezo na mazoezi ya mwili ili kuimarisha afya zao, kudumisha mshikamano kazini na kuongeza ufanisi katika kutekeleza majukumu yao.
Bonanza hilo ni sehemu ya juhudi za Wizara ya Madini na taasisi zake za kuhamasisha maisha yenye afya bora miongoni mwa watumishi, sambamba na kujenga mazingira yanayochochea umoja na ushirikiano kazini.
.jpeg)
.jpeg)


.jpeg)



0 Comments