Makamu Mkuu wa Chuo cha Taaluma, Tafiti na Ushauri wa Kitaaluma wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Prof. Robert Mashenene, amewataka wazazi na walezi kuwafundisha watoto matumizi sahihi na salama ya mitandao ya kijamii ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza.
Prof. Mashenene amesema wazazi wanaowapa watoto simu janja wanapaswa kuwaelekeza kuhusu mambo yanayopaswa na yasiyopaswa kufanywa wanapotumia mitandao ya kijamii, pamoja na namna ya kutumia teknolojia ya Akili Unde (AI) kwa manufaa ya masomo yao.
Ametoa wito huo katika Mahafali ya 26 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Green Acres jijini Dar es Salaam yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.
Aidha, amewashauri wazazi kuwashirikisha watoto katika shughuli za nyumbani na za uzalishaji mali, ikiwemo kupika, kufua na kufanya biashara, ili kuwajengea ujuzi wa maisha na kupunguza muda mwingi wanaotumia kwenye simu.
Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Green Acres Sekondari, Jonathan Kasabila, amesema wazazi wanapaswa kuweka utaratibu maalumu wa matumizi ya simu kwa watoto wanapokuwa nyumbani, pamoja na kuwaelimisha kuhusu matumizi sahihi ya vifaa hivyo na muda unaofaa kuvitumia.

.jpeg)

0 Comments