TRA MSHINDI WA KWANZA MARA 10 MFULULIZO WA TUZO ZA NBAA



MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeibuka mshindi wa kwanza kwa mara ya 10 mfululizo wa Tuzo za uandaaji bora wa vitabu vya hesabu zinazotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi Tanzania (NBAA) katika kundi la Taasisi za Wakala wa Serikali wanaotumia viwango vya kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta ya Umma (IPSASs).

Tuzo hizo zimeatolewa leo Novemba 26, 2026 katika Hoteli ya APC Mbweni Jijini Dar es Salaam ambapo kushinda kwa TRA ni kutokana na umahiri wa Idara ya Fedha katika uandaaji wa vitabu vya hesabu.

Awali akizungumza katika hafla ya utoaji wa Tuzo hizo mgeni rasmi ambaye ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Nsubili Joshua amezipongeza taasisi zilizoshinda na kutoa changamoto kwa taasisi nyingine kuwa mahiri katika eneo la kuandaa hesabu kwa viwango vya kimataifa.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments