UZOEFU NA VIPAJI: CHUMA CHAKAVU KUSHUKA DIMBANI

                               

Timu ya Chuma Chakavu (Singida All Stars) inatarajiwa kuwa na ratiba yenye ushindani mkubwa mwishoni mwa wiki hii, ikijiandaa kushuka dimbani katika michezo mitatu tofauti ya kirafiki itakayochezwa Novemba 28 na 29, 2026.

Michezo hiyo inatajwa kuwa sehemu muhimu ya kuendeleza mshikamano, kudumisha utimamu wa wachezaji na kuimarisha utamaduni wa ushindani ndani ya kikosi hicho kinachounganisha uzoefu, vipaji na mapenzi ya dhati kwa mchezo wa soka.

Katika mchezo wa kwanza utakaochezwa Jumamosi, Novemba 28, 2026, kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Uwanja wa Magereza, Chuma Chakavu itakuwa na kibarua dhidi ya Uhuru Veterans, mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani wa kiufundi na uzoefu kutoka pande zote mbili.

Baadaye siku hiyo hiyo, kikosi hicho kitarejea dimbani saa 10:00 jioni katika Uwanja wa Mandela, kuwakabili wenyeji Best Maridadi Veterans, kabla ya kuhitimisha ratiba yake Jumapili, Novemba 29, kwa mchezo dhidi ya Moshi Combine, inayounganisha Moshi Veterans na Ushirika Veterans.

UZOEFU, VIPAJI NA MSHIKAMANO NDIO SILAHA YA CHUMA CHAKAVU

Chuma Chakavu si kikosi kinachotazama soka kama mchezo wa matokeo pekee, bali pia kama jukwaa la kuendeleza urafiki, mshikamano, afya na kuthamini mchango wa wachezaji katika maendeleo ya mchezo huo.

Kupitia falsafa ya umoja na nidhamu, timu inalenga kuonesha kwamba umri si kikwazo cha kuendelea kuwa sehemu ya ushindani wa soka, mradi kuwepo kwa ari, maandalizi na kujituma.

Kwa kikosi hicho, kila mchezo ni fursa ya kuonesha ubora wa kiufundi, uzoefu wa kimchezo na thamani ya kucheza kama timu moja.

WITO KWA WACHEZAJI

Uongozi wa kikosi unawakumbusha wachezaji wote kuzingatia muda wa michezo, nidhamu na kuhakikisha wanavaa jezi rasmi za timu katika michezo yote iliyopangwa.

Ushiriki wa kila mchezaji ni sehemu muhimu ya kuimarisha taswira na heshima ya Chuma Chakavu ndani na nje ya uwanja.

CHUMA CHAKAVU – UZOEFU UNAONGOZA, VIPAJI VINANG'ARA, UMOJA UNATUTAMBULISHA!

Pamoja tunashinda, pamoja tunajenga historia ya soka.

BANDOLA MEDIA
Great Service Guaranteed.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560

Post a Comment

0 Comments