Bocco na Chikwende hizi Sababu za Kuikosa Mechi Ya Simba Na Ac Vita Congo

Kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes leo Februari 10 kinatarajiwa kuendelea na safari kuelekea Congo kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ni wa hatua ya makundi.

Jana, Februari 9 msafara wa wachezaji pamoja na benchi la ufundi waliweka kambi kwa muda Addis Ababa baada ya kuwasili hapo wakitokea Bongo, hivyo leo watamalizia ngwe ya safari ya mwisho.

Katika msafara huo ni nyota wawili ambao wamebaki Bongo ambao ni Perfect Chikwende yeye ni maalumu kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara  Kwa sababu amesajiliwa  round ya pili kutoka platinam amabayo ilitolewa na simba kwenye mashindano ya clabu bingwa barani africa msimu huu 2020-2021 kwahiyo hatulusiwa kutumikia clabu mbili kwenye mashindano ya clabu bingwa msimu huu.

Na nahodha John Bocco ambaye anasumbuliwa na majeraha aliyopata kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum. 

Hivyo nyota hao wawili wataukosa mchezo huo. Huku nyota Jonas Mkude ambaye alikuwa nje akitumikia adhabu ya utovu wa nidhamu yupo ndani ya kikosi.

Simba itatupa kete yake ya kwanza Februari 12 dhidi ya AS Vita ya Congo inayonolewa na Florent Ibenge ambaye anazijua mbinu za Simba.

Waliwahi kukutana kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi msimu wa 2018, Simba ililala mabao 5-0 na kipa alikuwa ni Aishi Manula, zama za Patrick Aussems ambaye yupo zake ndani ya AFC Leopards ya Kenya.

Gomes amesema:"Tunatambua utakuwa mchezo mgumu ila kazi yetu ni kupambana kusaka ushindi ndani ya uwanja na inawezekana,".

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments