BWALYA:TUMEKUJA KUFUATA USHINDI TANZANIA KWA SIMBA

 

NYOTA wa Al Ahly, Walter Bwalya amesema kuwa wamekuja Dar kwa lengo moja la kusaka ushindi mbele ya Simba kwenye mchezo wao wa hatua ya makundi ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Al Ahly ambao ni wababe wa soka ndani ya Afrika wakiwa ni washindi wa tatu kwenye Klabu Bingwa Duniani wanatarajiwa kumenyana na Simba, Uwanja wa Mkapa, Februari 23.

Kwa sasa kwenye kundi A, Al Ahly wanaongoza kwa idadi ya mabao matatu huku Simba wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi tatu baada ya kufungua pazia kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita, mchezo uliochezwa DR Congo.

 Bwalya amesema kuwa wanawatambua vizuri wapinzani wao hivyo hawatawapa shida kupata matokeo ndani ya uwanja.

Tunawatambua Simba uimara wao na pale ambapo wanakosea hivyo tumekuja Dar kwa lengo moja la kusaka ushindi na hilo linawezekana kwa kuwa tupo imara.

Nitapambana nami pia kuweza kuifunga Simba ili kuweze kufanikisha malengo ya Klabu ambayo ni kutwaa ubingwa wa Afrika,” amesema.

Bwalya aliibuka ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Nkana ya Zambia na iliwahi kucheza na Simba kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa ilitolewa Uwanja wa Mkapa hatua ya mtoano kwa kufungwa mabao 4-3.

Walipokuwa nyumbani, Nkana ilishinda 2-1 na zilipokuutana Uwanja wa Mkapa, Simba ilishinda mabao 3-1. 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments