Recent-Post

GURDIOLA:SINA MTU MAALUMU WA KUPIGA PENALTI

Kocha  Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kwa sasa hakuna mchezaji ambaye atakuwa na jukumu la kupiga penalti za timu hiyo kwenye mashindano yake yote.

Kwa sasa jukumu hilo amekabidhiwa kwa muda nyota Rodri raia wa Hispania baada ya wapigaji wa penalti ambao ni Sergio Arguero kutokuwa ndani ya uwanja kwa muda kutokana na kusumbuliwa na majeraha huku mshambuliaji wake Hugo LIoris akishindwa kuonyesha makeke yake ya kutupia.

Rodri alifanya hivyo kwa kupiga penalti yake ya kwanza Uwanja wa City Of Manchester, wakati wakishinda mabao 3-0 dhidi ya Spurs baada ya kujitolea kupiga penalti ndani ya kikosi hicho kinachopewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England uliopo mikononi mwa Liverpool inayokwenda kwa mwendo wa kusuasua.

Rodri alifunga penalti dakika ya 23 huku mabao mengine mawili yakitupiwa kimiani na Likay Gundogan  dakika ya 50 na 66 na kuifanya Spurs ya Kocha Mkuu, Jose Mourinho kuacha pointi tatu jumla mbele ya City.

Ni penalti 10 ambazo City iliweza kufunga kwenye jumla ya penalti 18 ambazo imezipata jambo ambalo lilimfanya Guardiola kufikiria kumpa jukumu la upigaji wa penalti kipa wake Ederson kutokana na uimara wake wa kupiga pasi akiwa uwanjani.

Guardiola amesema:"Ninafurahi kuona kwamba Rodri ameweza kuchukua jukumu la kupiga penalti na kufunga hilo ni furaha kwangu naamini na kwake pia kwa kuwa ametimiza majukumu yake. Unajua ukishindwa kufunga penalti wakati unahitaji ubingwa lazima uumie.

Kwa sasa sina mtu maalumu ambaye ana jukumu la kupiga penalti ndani ya kikosi changu, huo ni uhalisia na ipo hivyo kwa sasa hakuna mpigaji penalti," amesema.

City kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 53 huku Spurs ikiwa nafasi ya 9 na pointi 36 na watetezi Liverpool wapo zao nafasi ya nne na pointi zao 40. 

Post a Comment

0 Comments