Halima Mdee aachiwa huru kesi ya kutoa lugha chafu kwa Magufuli

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dar es Salaam Kisutu imemwachia huru mbunge wa viti Maalum, Halima Mdee katika kesi ya jinai iliyokuwa ikimkabili ya kutoa lugha chafu dhidi ya Rais John Magufuli.

Hukumu hiyo imetolewa leo Alhamisi Februari 25, 2021 na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba aliyekuwa akiisikiliza kesi hiyo.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Simba amesema kuwa upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake watatu umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa bila kuacha mashaka yoyote.

"Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa bila kuacha mashaka. Hivyo mshtakiwa hana hatia ya makosa na mahakama hii inamuachia huru," amesema Hakimu Simba.

Katika kesi hiyo, mbunge huyo wa zamani wa Kawe kupitia Chadema  alikuwa akikabiliwa na shtaka moja la kutoa lugha chafu dhidi ya Rais Magufuli.

Pamoja na mambo mengine kwa mujibu wa hati ya mashtaka alikuwa akidaiwa kusema kuwa Rais Magufuli anaongea hovyo hovyo, anatakiwa  afungwe  breki,  kauli zilizodaiwa na upande wa mashtaka kuwa ni za udhalilishaji dhidi ya Rais na kwamba maneno hayo yangeweza kusababisha uvunjifu wa amani.


TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments