Recent-Post

Jiji la Dar es Salaam kuvunjwa

Dar es Salaam. Rais  wa Tanzania, John Magufuli amesema Serikali ina mpango wa kuvunja Jiji la Dar es Salaam na kuchagua manispaa moja katika jiji hilo itakayopandishwa hadi na kuwa Jiji lengo likiwa kupunguza gharama zisizokuwa za lazima.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akizindua daraja la juu la Ubungo leo Jumatano Februari 24, 2021.

“Ninategemea kuvunja Jiji la Dar es Salaam ili tutengeneze jiji la eneo fulani tunaweza kuifanya Ilala ndio iwe jiji itategemea na namna mambo yatakavyokwenda lakini kuwa na madiwani ambao wanakaa hapa juu wanachangiwa fedha na hawana miradi ya maendeleo hili nitalikataa.

Tunataka Manispaa moja katika jiji la Dar es Salaam ndio ipandishwe hadhi iwe jiji halafu nyingine ziwe manispaa. Jiji la Dar es Salaam litaendelea kuwepo lakini tutachukua eneo fulani na ninafikiri Ilala inafaa kuwa jiji maana ndio ipo katikati, Ubungo itasubiri maana barabara bado hazijatengenezwa,” amesema Rais Magufuli.

Amewataka viongozi ambao walijiandaa kuwa mameya wa jiji wajue hilo limekwisha.

Haiwezekani unakuwa na madiwani wamekaa tu wanatengewa bajeti hizo fedha ni vizuri zikapelekwa kwenye miradi ya maendeleo ya barabara hayo ni matumizi bora ya fedha za walipakodi kwa hiyo mjiandae kisaikolojia meya atapatikana katika manispaa ya Ilala, amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments