Recent-Post

Kama hujachukua hati miliki ya ardhi hii inakuhusu

Geita. Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amewataka wananchi wenye hati miliki za ardhi lakini hawajazichukua wafanye hivyo kwa kuwa wizara hiyo si eneo la kutunzia hati.

Ameyasema hayo leo Jumanne  Februari 16, 2021 wakati akizungumza na watumishi wa idara ya ardhi wa halmashauri zote za mkoa wa Geita , kampuni ya upimaji ardhi pamoja na wananchi waliofika kukabidhiwa hati zao.

Ametoa kauli hiyo kutokana na wananchi nane kati ya 25 ndio waliofika kuchukua hati miliki sambamba na kuhudhuria hafla hiyo.

Aliwataka wananchi kujenga utamaduni wa kuchukua hati miliki za ardhi badala ya kuziacha kwa wataalam na kwamba Wizara itaanza kuwatoza gharama za kuwatunzia ili wawe wanajitokeza kwa wakati na kuanza kulipa kodi ya ardhi.

Katika hatua nyingine, Mabula amezitaka idara za ardhi kujipanga na kuweka mpango wa kuandaa hati miliki kwa wingi tofauti na sasa ambapo takwimu zinaonyesha Mkoa huo kwa kipindi ha miezi sita wameandaa hati miliki 386 pekee.

"Kuandaa hati 386 kwa kipindi cha mwezi mzima ni aibu kwa kuwa viwanja ni vingi na kutotoa hati kunachangia mapato ya Serikali kutokusanywa kwa wakati,  wenzenu Ilemela halmashauri kwa mwezi wanaandaa hati miliki 300 nyinyi Mkoa mzima ndio mnaandaa kwa miezi sita" amesema Mabula.

Post a Comment

0 Comments