Recent-Post

KATWILA ATAMBA KUINUSURU IHEFU

Ushindi dhidi ya Ruvu Shooting umemuibua kocha mkuu wa kikosi hicho, Zubery Katwila ambaye ametamba kuwa ndiyo wameanza rasmi safari ya kujiondoa mkiani mwa msimamo wa ligi ili kusaka nafasi ya kusalia Ligi Kuu.

Katwila Ijumaa aliiongoza Ihefu kupata ushindi wake wa nne msimu huu baada ya kucheza michezo 19, na kufanya kikosi hicho kufikisha pointi 16 zinazowaweka kwenye nafasi ya 16 kwenye msimano wa ligi.

Akizungumzia mipango yao, Katwila alisema: “Tunajua wazi kwamba bado hatupo kwenye nafasi nzuri sana kwenye msimamo wa ligi.

Hivyo tumeanza, na tutaendelea kupambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri katika michezo yetu ijayo ili kuweza kujinusuru na janga la kushuka daraja ili kikosi chetu kishiriki Ligi Kuu msimu ujao.


Post a Comment

0 Comments