KAZE:NILIWASOMA MTIBWA SUGAR ZANZIBAR

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa ushindi walioupata mbele ya Mtibwa Sugar umetokana na kuwasoma wapinzani hao kwa muda mrefu ndani na nje ya uwanja.

Jana, Februari 20 Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Bao pekee la ushindi lilipachikwa na kiungo Carlos Carlinhos ambaye alitokea benchi na kufunga bao hilo dakika ya 73.

Ushindi huo unaifanya Yanga kujenga ngome nafasi ya kwanza ikiwa na jumla ya pointi 49 baada ya kucheza jumla ya mechi 21.

Kaze amesema:"Niliwasoma wapinzani wangu kupitia mashindano ya Kombe la Mapinduzi yaliyofanyika visiwani Zanzibar ambapo nilijua wapi nitaweza kupata ushindi juu ya kikosi hicho.

"Niliwaambia wachezaji wangu kwamba ni lazima wapambane na watumie akili kusaka ushindi kwa kuwa wachezaji ambao wanacheza nao wana uzoefu na uwezo wa kusaka ushindi ndani ya uwanja.

Katika hilo tumefanikiwa na kushinda hivyo ni mwendelezo wetu wa kuyafuata mafanikio ndani ya uwanja," amesema.

Mtibwa Sugar mchezo wake uliopita ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Ihefu imepoteza mbele ya Yanga ambayo ilitoka kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Kagera Sugar.

Pia kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana Uwanja wa Jamhuri ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0. Jumla imefungwa mabao mawili na kuacha pointi sita kwa Yanga.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments