Recent-Post

KIM POULSEN, KOCHA MKUU WA TAIFA STARS

 

Kim Poulsen raia wa Denrmark ameteuliwa rasmi na Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kocha huyo ambaye aliwahi kuwa mshauri kwenye timu ya taifa ya vijana amesaini dili la miaka mitatu anachukua mikoba ya rasmi Ettiene Ndayiragije raia wa Burundi ambaye alifikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake na Stars.

Ndayiragije alifikia hatua hiyo Februari 11 ambapo ilimshukuru na kumtakia kila la kheri atakakokwenda.

Taarifa rasmi iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa kocha huyo ambaye aliwahi pia kuinoa Stars mwaka 2012 na 2013 anachukua nafasi ya Ndayiragije ambaye alijiunga na Stars, Julai 2019. 

Post a Comment

0 Comments