JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa wachezaji wake walitengeneza nafasi nyingi kwenye mchezo wao wa Merseyside Derby dhidi ya Everton licha ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-0.
Dakika 90 zilikamilika kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu England kupiga jumla ya mashuti 15 na sita yalilenga lango huku wapinzani wao Everton wakipiga jumla ya mashuti 9 na sita yalilenga lango.
Mbali na hilo pia umiliki wa mpira kwa Liverpool iliyo nafasi ya 6 na pointi 40 baada ya kucheza mechi 25 ilikuwa ni asilimia 72 huku Everton iliyo nafasi ya 7 na pointi 40 abaada ya kucheza jumla ya mechi 24 ikiwa ni asilimia 28.
Klopp amesema:"Tulicheza vizurri kwenye umiliki pia ilikuwa hivyo hata kushambulia kwetu ilikuwa zaidi yao ila vijana wameshindwa kutumia nafasi, hakuna namna tunajipanga kwa ajili ya wakati ujao,".
0 Comments