Recent-Post

MANCHESTER UNITED YAMPIGA MTU 9-0

 


KOCHA Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskajer amesema kuwa kujiamini kwa wachezaji wake kumewafanya waweze kupata ushindi kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England, usiku wa kuamkia leo.

Manchester United iliwalaza na viatu wapinzani wao Southampton kwa kushinda mabao 9-0 jambo lililowafanya wasepe na pointi tatu mazima.

Ole amesema:"Ninadhani kwamba hali ya kujiamini kwa wachezaji imechangia haya matokeo mazuri ndani ya uwanja wanastahili pongezi,". 
 
Kwenye mabao hayo ambayo yalifungwa Uwanja wa Old Trafford yote 9 ni bao moja lilikuwa la kujifunga huku Martial pekee akitupia mabao mawili.

Watupiaji walikuwa ni Aaron Wan-Bissaka dk 18, Marcus Rashford dk 25, Jan Bednareck dk 34 Og, Edinson Cavan dk 39, Anthony Martial dk 69 na 90, Scott Mc Tominay 71,Bruno Fernandes 87 na Daniel James 90+3.

Wachezaji wawili wa Southampton walionyeshwa kadi nyekundu ilikuwa ni kwa Alex Jankewitz dakika ya 2 na Jan Bednarek dakika ya 86.

Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kufikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza jumla ya mechi 22 kinara ni Manchester City  wenye pointi 44 na wamecheza jumla ya 20.

Mabingwa watetezi Liverpool wapo nafasi ya tatu na ina pointi 40 ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 na Southampton ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 29.

Post a Comment

0 Comments