Mwanaharakati aeleza alivyowawezesha wanawake kibiashara wakati wa Corona


Dar es Salaam. Mwaka 2020 haukuwa salama katika kila nyanja tangu kwenye uchumi, kijamii na kisiasa, kwani nchi nyingi zilisimamisha shughuli za wazi zinazohusisha mikusanyiko ya watu wengi kutokana na maambukizi ya Corona.

Lakini Janeth Mawinza ambaye ni mwanaharakati wa kupinga unyanyasaji wa wanawake anayetoka taasisi ya Wanawake katika Jitihada za kimaendeleo (Wajiki) amesema walitumia changamoto hiyo kuwa fursa ya kuwainua kiuchumi wanawake.

Akizungumza na Mwananchi karibuni Dar es Salaam, Mawinza ambaye ni mkurugenzi wa Wajiki anasema walishirikiana na taasisi ya Soma kuamzisha mradi wa Mshikamano Hub ambao ulisaidia wanawake wakati wa majanga hasa Corona.

Wanawake waliathirika zaidi kwa sababu walikuwa wakipanga biashara zao wateja hawakwenda; kwa mfano mwanamke muuza ndizi wateja waliogopa kwamba anaweza kuwaambukiza Corona.

Kwa hiyo tulitafuta njia ya kutoa sauti na hapo wenzetu Soma waliuona na kuanzisha mradi ambapo sasa mteja halazimiki kwenda kwa mwanamke anayefanya biashara pale. Tuliwatumia madereva wa bodaboda kufikisha bidhaa kwa wateja wao,” anasema.

Hawakuishia hapo, kwani pia walianzisha mradi wa kutengeneza pilipili na karanga ili kuwasaidia wanawake kujipatia kipato wakati wa Corona huku wakipinga ukatili.

Tukaanzisha mradi wa kutengeneza pilipili, lakini kwenye kifungashio tunaweka karatasi yenye ujumbe wa kampeni yetu. Pia tulitengeneza karanga zenye ujumbe huo,” anasema.

Pia anasema mradi huo uliwawezesha wanawake kutoa taarifa ya matukio ya ukatili kwani katika kipindi cha kufungiwa kutokana na ugonjwa wa Corona baadhi ya wanawake waliofanyiwa vitendo vya ukatili hawakuweza kutoka kwenda kutoa taarifa ka kuhofia maambukizi.

Kwa upande mwingine, Mawinza anasema waliendelea kutoa elimu ya kupinga ukatili wa wanawake katika kipindi cha Corona kwa kuweka maturubali na vitakasa mikono na kuweka mabango yenye ujumbe ya kupinga ukatili huo.

Tulitafuta njia mbadala kwa kuweka matrurubali na kuweka maji ya kunawa na vitakasa mikono na kuweka mabango ya kuelimisha kuhusu ukatili wa ngono ili atu wajikinge. Pia tulitengeneza barakoa na sabuni ambazo pia tuliweka ujumbe wa kampeni ya rushwa ya ngono. Mtu atumie bidhaa lakini pia apate ujumbem,” anasema.

Miongoni mwa wanawake walionufaika na taasisi ya Wajiki ni Belina Mgalula anayeishi Mwananyamala Dar es Salaam.

Anasema mapema mwaka 2020 baada ya Serikali kutangaza kuwepo kwa ugonjwa huo, alikutana na taasisi ya Wanawake katika Jitihada za kimaendeleo (Wajiki) ambayo inafanya kampeni za kupinga ukatili na kuinua wanawake kiuchumi.

Wajiki walitukusanya baadhi ya wanawake na kutufundisha biashara ya kuuza karanga za mayai na kutengeneza pilipili . Pia tulifundishwa kutengeneza sabuni za maji na vitakasa mikono. Baada ya kutengeneza tunavikweka kwenye vifungashuio tunavyonunua soko la Kariakoo na kupeleka kwa wateja,” anasema Mgalula.

Wakati huo huo anasema pia walikuwa wakiendelea na kampeni za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kuweka ujumbe kwenye bidhaa wanazouza.

Biashara imekuwa nzuri kiasi kwakmba kwa siku nauza pilipili ya Sh50,000 kwa kupeleka kwenye maduka ya reja reja na bucha za nyama maeneo mbalimbali Dar es Salaam. Nashukuru kwa sababu kila mara soko linaongezeka, napata wateja wanaotaka niwapelekee.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments