Recent-Post

NAMUNGO YASAINI DILI LA MWAKA MMOJA NA SportPesa

KLABU ya Namungo FC imeingia mkataba wa mwaka mmoja na Kampuni ya michezo ya kubashiri Tanzania, SportPesa wenye thamani ya shilingi milioni 120.

Mkurugenzi wa SportPesa Tanzania, Abbas Tarimba amesema kuwa wameamua kufanya hivyo kutokana na kuridhishwa na mwenendo wa timu hiyo inayoshiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Tumeridhishwa na mwenendo wa Namungo FC kwenye Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na namna ambavyo wanapambana kuweza kupeperusha bendera ya Tanzania.

Tunaamini kwamba huu ni mwanzo na ina nafasi ya kufanya vizuri kimataifa hivyo tunawatakia kila la kheri na tutazidi kuwa pamoja katika sekta ya michezo. 

Mwenyekiti wa Namungo FC,Hassan Zidadu amesema kuwa wanashukuru kwa udhamini huo na wanaamini kwamba utawapa nguvu ya kupamba zaidi kitaifa na kimataifa.

Tunashukuru kwa ajili ya udhamini wa ambao wameweza kufanya kwetu na tunaahidi kupambana zaidi kwa ajili ya mechi zetu za kitaifa na kimataifa pia. 

Post a Comment

0 Comments