Recent-Post

NYOTA KUTOKA SINGIDA ,AKAELEKEA KANDA YA ZIWA NA SASA YANGA PRINCESS AFIKIRIA MABAO 100


Aisha  Mashaka, 'Ashamabao' mshambuliaji wa timu ya Yanga Princess amesema kuwa kwenye kila mashindano huwa anafikiria kufunga mabao 100.

Kwa sasa Kwenye Ligi ya Wanawake Tanzania,  Asha ni namba mbili kwa utupiaji ambapo Oppa Clement wa Simba Queens na Fatma Mustapha wa JKT Queens namba moja wakiwa wametupia mabao 20.

Yeye Asha ikiwa ni msimu wake wa kwanza ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Edna Lema ametupia mabao 15.

Kikosi cha Yanga Princess kinaongoza Ligi Kuu ya Wanawake baada ya kucheza mechi 11 na kibindoni kina pointi 31.

Asha amesema:"Huwa nafikiria kufunga mabao kuanzia 100 jambo ambalo linanifanya nazidi kupambana ndani ya Uwanja.

Post a Comment

0 Comments