Jana asubuhi, siku moja baada ya kuteuliwa na Rais John Magufuli, Dk Bashiru Ally aliapishwa kuwa Balozi na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Dar es Salaam, huku akiahidi mambo matatu kwa kiongozi mkuu huyo wa nchi.
Aliteuliwa kushika wadhifa huo baada ya kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi.
Nyota ya Balozi Bashiru ilianzia wapi? Unaweza kujiuliza swali hili lakini unaweza kusema iliendelea kung’ara kutokana na mijadala yake ya hoja akiwa na wanazuoni wengine.
0 Comments