SIMBA WAFICHUA MBINU YA KUWAMALIZA WAARABU KWA MKAPA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa una mbinu mpya na kali ambayo wanaamini kwamba itawarahisishia kupata ushindi kwenye mchezo wao wa kimataifa, kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Mchezo huo ambao mashabiki 30,000 wataruhusiwa kushuhudia Uwanja wa Mkapa ikiwa ni kwa ajili ya kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi ya Corona unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja.

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez, amesema tayari wana mbinu kali ambayo itawasaidia kupata ushindi kwenye mechi hiyo dhidi ya Al Ahly.

 Barbara ameongeza kuwa mbinu ambayo itawapa ushindi katika pambano hilo la Ligi ya Mabingwa Afrika ni kuwafanyia uchambuzi wa kina wapinzani wao kwa kufahamu maeneo dhaifu ambayo yatawapa picha ya namna ya kukabiliana nao. Kazi hiyo inaongozwa na mtaalamu wao, Mzimbabwe, Culvin Mavhunga.

 

Kuhusiana na mechi yetu na Al Alhy, kitu kikubwa ambacho tunafanya ni uchambuzi wa wapinzani wetu ambao unatuonesha udhaifu wao.

 

Uchambuzi huo ni wa kina na ndiyo maana tumewekeza sana katika kipengele hicho kwani inatupa picha ya kuwafahamu wapinzani wetu na sisi juu ya kikosi chatu kilivyo na sehemu gani ambazo tunaweza kuwafunga,” alimaliza Barbara.


Itakuwa ni Februari 23, Simba itakapowakaribisha Waarabu wa Misri, Uwanja wa Mkapa timu zote zina pointi tatu kwa kuwa mechi zao za ufunguzi zilishinda, Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya AS Vita na Al Ahly ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Al Merrikh.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments