Akizungumza na Spoti Xtra, Kapombe alisema kuwa kila siku wamekuwa wakikumbushana kuhusu malengo yao kimataifa jambo ambalo linawapa nguvu ya kuzidi kupambana.
Kila wakati tunapokuwa pamoja kambini, mazoezini tunakumbushana kuhusu malengo ya timu hivyo jambo hilo linatupa nguvu ya kufanya vizuri kimataifa, mashabiki watupe sapoti tuna amini tutafikia malengo yetu,” alisema.
Kapombe ni chaguo la kwanza la Gomes pia hata zama za Sven Vandenbroeck ambaye kwa sasa yupo na Klabu ya FAR Rabat alikuwa chaguo la kwanza na alicheza mechi zote za kimataifa ikiwa ni pamoja na ile ya Plateau United ya Nigeria na FC Platinum ya Zambia.
0 Comments