Recent-Post

VIONGOZI WA SERIKALI WAKUMBUSHWA KUTEKELEZA MAELEKEZO YA RAIS MAGUFULI.

 

Mwandishi Wetu, MorogoroKatibu 

Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amewakumbusha viongozi wa serikali kutekeleza maelekezo ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa Juni 4, 2020, kuhusu kutangaza shughuli za Serikali.

Dkt. Abbasi ameyasema hayo mjini Morogoro jana ambapo alikuwa akitoa mada wakati wa mkutano wa mwaka wa washitiri unaohusisha taasisi mbalimbali za Serikali ulioandaliwa na TBC.

"Katika kipindi hiki cha pili Serikali ya Awamu ya Tano itawatathmini maafisa habari lakini pia na viongozi wao maana wapo baadhi ya watendaji wakuu wa taasisi ndio siku zote wanakwamisha utoaji wa taarifa za utekelezaji wa Serikali katika maeneo yao bila sababu za maingi, ni urasimu tu basi," alisema Dkt. Abbasi na kuzitaka ofisi za umma kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ili wananchi wajionee kwa macho kazi inayoendelea.

Akitoa tathmini ya awali Dkt. Abbasi alisema kuna mabadiliko makubwa katika namna idara mbalimbali za Serikali zinavyotumia ubunifu katika kutangaza shughuli za Serikali.

"Kwa ujumla tuko vizuri lakini hatujafika tunapopataka. Tuendelee kuongeza ubunifu, kuongeza vifaa na kuhakikisha habari zinazotolewa zinasheheni takwimu na ushahidi wa kuonesha maendeleo yanayotokea," aliongeza

Mwisho.

Post a Comment

0 Comments