Dar es Salaam. Ni simanzi. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad kufariki dunia leo Jumatano Februari 17, 2021 katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.
Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi ametangaza siku saba za maombolezo huku Rais John Magufuli naye akitoa salamu za pole.
Viongozi mbalimbali pia wametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mwenyekiti huyo wa chama cha ACT-Wazalendo ambaye kabla ya kujiunga na chama hicho alikuwa katibu mkuu wa CUF.
Kupitia kurasa za mitandao ya kijamii Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Mwigulu Nchemba amesema, “pumzika kwa amani mzee wetu Maalim Seif, makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. Natoa pole kwa familia, Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na Watanzania wenzangu wote. Pumzika kwa Amani.”
Mwanasheria Fatma Karume amesema, “inna lilahi wa inna ilayhi rajiun Nimehuzunika sana kusikia Maalim amefariki. He was a good man and a good friend.”
Kwa upande wake kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe alinukuu maneno aliyozungumza Maalim Seif mwaka 1987 katika viwanja vya Tibirizi mjini Pemba.
Nipo nanyi sasa hivi, ninawaahidi kuwa nitakuwa nanyi nikiwa ndani ya Serikali au nje ya Serikali. Nitakuwa nanyi nikiwa ndani ya chama au nje ya Chama.”
Seif Sharif Hamad, Desemba 1987 Viwanja vya Tibirinzi, Pemba – Zanzibar.
0 Comments