WANNE WA AZAM FC KUIKOSA TANZANIA PRISONS KESHO

NYOTA wanne wa kikosi cha kwanza cha Azam FC kinachonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kesho wanatarajiwa kuukosa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Mchezo huo ulibadilishiwa tarehe kwa kuwa Uwanja wa Azam Complex unatumiwa na Namungo FC kwenye mechi za kimataifa ambapo leo Februari 21 watacheza dhidi ya 1 de Agosto ya Angola ambao ni mchezo wa Kombe la Shirikisho.

Hivyo badala ya mchezo huo wa ligi kuchezwa leo, utachezwa kesho majira ya saa 1:00 usiku, Uwanja wa Azam Complex.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa katika wachezaji ambao hawapo kwenye mpango wa Lwandamina ni watatu.

"Wachezaji watatu hawatakuwa sehemu ya kikosi cha kesho dhidi ya Tanzania Prisons kwa kuwa wanasumbuliwa na majeraha ikiwa ni pamoja na Salum Abubakary,'Sure Boy', Yahya Zayd pamoja na Frank Domayo hawa wanasumbuliwa na majeraha.

"Obrey Chirwa yeye aliumia kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Simba ila kwa sasa anaendelea vizuri na ameanza mazoezi mepesi hapo kazi itakuwa mikononi mwa mwalimu kuamua kumtumia ama la.

"Kuhusu maandalizi kila kitu kipo sawa na tutapambana kusaka matokeo chanya,". 

Post a Comment

0 Comments