WASHILIKI WA SIMBA SUPER CUP WAKUBALI MZIKI WA TIMU YA SIMBA


 

Kiwango bora kilichoonyesha na Simba kwenye michuano ya Simba Super Cup kimezifanya klabu shiriki za michuano hiyo, TP Mazembe na Al Hilal kuivulia kofia Simba na kukiri kweli kikosi hiko kiko cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara kiko vizuri.

Katika michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Januari 27, na kufikia tamati Januari 31 Simba iliibuka bingwa baada ya kujikusanyia pointi nne katika michezo miwili waliyocheza.

Michuano hiyo, ilifanyika kwa lengo la kuziandaa timu shiriki na michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Akizungumzia kiwango cha Simba, Kocha mkuu wa Al Hilal Zoran Mamic amesema: “Tulipoteza mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Simba kwa mabao 4-1, licha ya kwamba kikosi chetu kiliwakosa nyota kumi wa kikosi cha kwanza na pia tulichelewa kufika Tanzania lakini ni wazi tunapaswa kukiri kuwa Simba walikuwa bora dhidi yetu.

 Wana kikosi kizuri, na faida ya kucheza nyumbani iliwabeba zaidi, namini watafanya vizuri kwenye michezo yao ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Naye mwakilishi wa benchi la ufundi la TP Mazembe Kabongo Ngadu alisema: “Tulipata nafasi ya kuutazama mchezo kati ya Simba na Al Hilal na pia kucheza dhidi yao, nikiri kuwa wana kikosi kizuri 

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments