YANGA YAMPIGIA HESABU NDEFU MTAMBO WA MABAO MZAWA

 

MESHACK Abraham, mshambuliaji wa kikosi cha Gwambina FC anatajwa kuwekwa kwenye rada za mabosi wa Yanga ili kuweza kuona uwezo wake kwenye mechi za ushindani.

Nyota huyo ambaye jina lake limetajwa na Kocha Mkuu, wa timu ya Taifa ya Tanzania, Kim Poulsen kwenye orodha ya  wachezaji watakaongia kambini Machi 8 kujiandaa na mechi za kufuzu Afcon alikuwa kwenye hesabu za kutua kikosini hapo ila dili lake likabuma.

Kwa sasa Yanga inapambana kurejea kwenye ubora huku ikiwa imekosa washambuliaji wenye uwezo wa kuwa na mwendelezo mzuri ndani ya uwanja, ambapo kwenye mechi 21 imefunga jumla ya mabao 34 na kinara ni winga Deus Kaseke mwenye mabao 6.

Michael Sarpong na Yacouba Songne ambao ni washambuliaji hawa wametupia mabao manne kila mmoja huku nyota Ditram Nchimbi akiwa ametengeneza pasi mbili za mabao.

Habari kutoka ndani ya Gwambina zimeeleza kuwa Yanga wanampigia hesabu nyota huyo.

"Yanga inahitaji huduma ya Abrahm ila kwa sasa itakuwa ngumu kwa kuwa dirisha la usajili limefungwa hapo itakuwa ni mpango ujao na kwa sasa wanachokifanya ni kumfuatilia kwenye kila mechi ambazo anacheza," ilieleza taarifa hiyo.
 
Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa tatizo lipo kwenye umaliziaji wa nafasi ambazo wanazitengeneza jambo ambalo atalifanyia kazi.

Ndani ya Gwambina FC, Abraham ametupia jumla ya mabao 7.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments