AZAM FC YATUMA UJUMBE KWA MABINGWA WATETEZI SIMBA

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa msimu huu hautatoka mikono mitupu kama ilivyokuwa msimu uliopita wa 2019/20.

 Ujumbe huo unaingia moja kwa moja kwa mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho pamoja na Ligi Kuu Bara, Simba ambao nao wameweka wazi kwamba wanahitaji kutetea mataji yao yanayopigiwa hesabu pia na vinara wa ligi, Yanga.

 Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit alisema kuwa malengo makubwa kwa msimu wa 2020/21 ni kutwaa moja ya taji kubwa na ikiwezekana yote mawili. 

Tuna kikosi kizuri chenye wachezaji makini ambao wanajituma ndani ya uwanja, kwa namna ambavyo ushindani unakwenda na namna tunavyopata matokeo mazuri hatutatoka mikono mitupu.


Malengo ni kuona tunatwaa mataji mawili ama moja kati ya haya makubwa lile la ligi pamoja na Kombe la Shirikisho, tunahitaji kurejea kimataifa na hilo linawezekana mashabiki watupe sapoti,” alisema.

 Kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya tatu imekusanya pointi 37 baada ya kucheza mechi 21 na kwenye Kombe la Shirikisho imetinga hatua ya 16 bora baada ya kushinda bao 1-0 dhidi ya Mbuni FC inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, itakutana na Polisi Tanzania, Uwanja wa Azam Complex.

Kinara wa utupiaji ni Prince Dube mwenye mabao saba ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na George Lwandamina.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments