BARCELONA WAONDOLEWA NA PSG KLABU BINGWA ULAYA

 

SARE ya PSG kufungana bao 1-1 dhidi ya Klabu ya Barcelona kwenye mchezo uliochezwa usiku wa kuamkila leo katika UEFA Champions League imewaondoa jumla Barcelona.

 Kylian Mbappe alifunga bao la kwanza kupitia njia ya penalti dakika 30 baada ya mechi hiyo kuanza huku Lionel Messi akifunga dakika saba kabla ya kukamilika kwa mechi hiyo.

 

 Kufuatia matokeo hayo Paris Saint Germain ilifuzu katika robo fainili ya kombe hilo. PSG iliishinda Barcelona kwa jumla ya mabao 5-2 nyumbani na ugenini baada ya kuilaza kwa magoli 4-1 katika uwanja wa Nou Camp mwezi Februari.

 

 Hii ni mechi ya 13 kati ya timu hizo mbili katika kombe la Klabu Bingwa Ulaya huku Barcelona ikishinda mara tano na PSG mara tano.

 

 Hii ni mara ya kwanza kwa mabingwa hao wa Uhispania kushindwa kufika robo fainali ya kombe hilo baada ya kufuzu kwa miaka 15 mfululizo.

 

 Hata hivyo mkufunzi wa klabu hiyo Ronald Koeman amesema kwamba jinsi walivyoyaaga mashindano hayo kunaweza kumshawishi raia huyo wa Argentina kundelea ushirikiano wake wa muda mrefu na klabu hiyo.

 

 

Leo {Messi} ameona kwa muda sasa kwamba timu hii inaimarika kutokana na mabadiliko tuliofanya”, alisema Koeman.

 

 

Hususan , tuna wachezaji wachanga wenye uwezo mkubwa. Hatma yetu siku zijazo itakuwa nzuri . Leo hawezi kuwa na wasiwasi wowote kuhusu hatma ya timu hii”.

 

 

Tunayaaga mashindano haya ya klabu bingwa kwa njia tofauti sana ukilinganisha na jinsi ilivyokuwa msimu uliopita.Katika mechi hii , tuliimarika na hbiyo ndio njia ya kufuata”.

 

Matokeo mengine
Liverpool 2-0 RB Leipzig

Borrussia Dortmund 2-2 Sevilla

Juventus 3-2 FC Porto

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments