CAF YATOA TAMKO KUHUSU AL MERRIKH KUDAI KUHUJUMIWA NA SIMBA

Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) limewaambia mabosi wa Al Merrikh kuwa waendelee na program zao kwa sasa wasahau pointi tatu ambazo walizokuwa wakihitaji kuzipata kutoka Simba.

Mabosi wa Al Merrikh walitua Caf Machi 21 kulalamika kuhusu jambo ambalo walieleza kuwa wamehujumiwa na Simba katika vipimo vya wachezaji wao.

Kwenye malalamiko hayo, Al Merrikh ambayo ilicheza na Simba, Machi 16 na kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0, wachezaji wake 8 ilielezwa kuwa wana Corona jambo ambalo walidai kwamba ni hujuma.

Barua ambayo wametumia Al Merrikh na Caf, jana Machi 28 imeeleza kuwa wanapaswa kuendelea na mipango yao kwa kuwa hakukuwa na hujuma zozote.

Barua hiyo imeeleza kuwa walipokea malalamiko hayo na utaratibu wa kupima Corona ulifuatwa na watu wa Simba hivyo kama hawajakubali kuhusu maamuzi hayo ni ruksa kwao kurejea tena Caf.

Kikosi cha Simba kinaongoza kundi A kikiwa na pointi 10, Al Merrikh wapo nafasi ya nne na ina pointi moja baada ya kucheza mechi nne, imelazimisha sare mbele ya Simba Uwanja wa Al Hilal na imepoteza mbele ya AS Vita na Al Ahly ambazo zote zimefungwa na Simba.

Kuhusu suala hilo Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa bado hajapewa taarifa kutoka kwa uongozi wa juu.

TUANDIKIE MAONI YAKO HAPA CHINI

Je, wewe ni Mfanyabiashara na Unatamani Kutangaza Bidhaa Zako Kupitia Tovuti/Blog Yetu? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia bandolaonline@gmail.com au WhatsaApp: + 255 766 365 560 au 0652 388 516

Post a Comment

0 Comments