Recent-Post

DEMBELE AANGUKA MAZOEZINI, HALI YAKE IMEREJEA KWENYE UBORA

 

Uongozi wa Klabu ya Atletico Madrid umesema kuwa mshambuliaji wao Moussa Dembele anaendelea vizuri kwa sasa kwa kuwa alipata tatizo kidogo kwenye msukumo wa damu.


Dembele kwenye mazoezi ya jana Machi 23 alidondoka ghafla wakati wakiwa katika mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Klabu ya Lyon alianza kuokolewa na wachezaji wenzake kabla hawajawaita wataalamu wa afya ndani ya Atletico Madrid.

Watendaji hao kazi wa Atletico Madrid kutoka kitengo cha afya walitumia muda mwingi kujaribu kumrudisha kwenye hali ya kawaida.

Ripoti zimeeleza kuwa nyota huyo mwenye miaka 24 aliweza kurejea kwenye hali yake ya kawaida kwa kuwa hakuwa na tatizo kubwa bali mgandamizo wa damu ulikuwa mdogo.

Post a Comment

0 Comments