Shilikisho la soka la kimataifa (FIFA), limefuta pingamizi la kutofanya kazi nchini Afrika kusini kwa aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga, Luc Eymael.
Eymael alifikwa na maamuzi hayo kutoka kwa Chama cha soka cha Afrika Kusini (SAFA), mwezi Julai mwaka jana.
Kutokana na kauli hiyo, Yanga walisitisha mkataba wa kocha huyo na kutakiwa kuondoka nchini haraka, jambo ambalo alilitekeleza huku mashauri mengine yakibaki kuwa chini ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF).
0 Comments